The River Conference of the Free Methodist Church

Sera ya TRC kutambua uwepo wa unyanyasaji wa kingono (Sexual Harassment Swahili)

UTANGULIZI

Imetayarishwa na The River Conference kwa kushirikiana na shirika la bima ya Brotherhood Mutual

WEKA WAZI SERA ZAKO ZA UNYANYASAJI

Sera za unyanyasaji wa ngono za shirika lako zinapaswa kuelezea kwa uwazi malengo yake ya kudumisha usalama na ukarimu mahali pa kazi. Mpango ulio wazi na andiko elekezi, zinasaidia kufafanua wazi jinsi sera hizi zinavyoweka taratibu zinazofaa katika kulinda maslahi ya shirika na wafanyakazi wake. Sera zilizo madhubuti zinapaswa kuwaelimisha wafanyakazi, na kuonyesha kwamba mashtaka ya unyanyasaji wa kingono yanapotolewa, huchuguzwa kabisa kikamilifu.

SERA ZENYE MSIMAMO MKALI HULINDA WATU NA HUDUMA

Huduma nyingi za Kikristo zinatakiwa kuwa na msimamo mkali dhidi ya unyanyasaji wa kingono mahali pa kazi. Kutofanya hivyo kunaweza kusababisha madhara yanayoweza kuleta athari katika nyanja mbalimbali, kibinafsi, kitaaluma, kisheria, na kumharibia mtu sifa zake na maadili yake; na kwa hivyo, athari hizi zinaweza kuharibu huduma ya shirika la Kikristo, kama vile kanisa, shule, au chuo. Sera madhubuti zilizowekwa wazi kwa maandishi ni msingi unaowezesha ustawi wa utamaduni wa uwazi na uwajibikaji.

UNDA SERA ZINAZOFAA

Mchakato wa uundaji wa sera zinazofaa, huanza kwa kufafanua wazi maana ya unyanyasaji wa kingono. Hata kama inaonekana ni jambo linaloeleweka kwa wengi, ni muhimu kusema wazi ni tabia zipi ambazo hazikubaliki mahali pa kazi.

“Sera za unyanyasaji wa kingono zinazofaa zinapaswa kuwaelimisha na kuwafundisha wafanyakazi kutambua unyanyasaji wa kingono na kutoa taarifa. Unapo wahimiza wafanyakazi kutoa taarifa za unyanyasaji, unaunga mkono kauli uliyoitaja katika sera yako, na kwa kufanya hivyo unaonyesha kwamba unyanyasaji huo hautavumiliwa,” maneno haya aliyasema Kathleen Turpin, makamu wa rais – idara ya Human Resources ya Brotherhood Mutual.

Tatizo la unyanyasaji wa kingono lipo kazini, kama (kwa kutajwa kabisa au kudokezwa) hutumika kama sharti la kupata ajira, au kama linatumiwa kama kigezo katika maamuzi kazini; kwa ujumla, unyanyasaji wa kingono huingilia utendaji wa kazi kwa kiwango kikubwa sana, na kujenga mazingira yanayotisha au kuleta uhasama kazini.

 

IKILETWA TUHUMA YA UNYANYASAJI WA KINGONO, ZIFUATAZO NI HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA KWA KUFUATA UTARATIBU ULIKO KWENYE KITABU CHA NIDHAMU CHA KANISA LA FREE METHODIST (TRC itaratibu na kusimamia tuhuma zote zinazotokea kwenye sehemu husika – conference)
 • TRC inaweza kupata ushauri wa kisheria kutoa mwongozo katika mchakato wa kuchunguza tuhuma.
 • Katika mchakato wa kushughulikia shtaka lolote la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mzee wa kanisa, CMC, au LMC, TRC / MEG, TRC itaagiza Kitabu cha Nidhamu kitoe
 • Vikao vyote virekodiwe. Kabla kikao hakijaanza, sema maneno yafuatayo, “Mkutano huu unarekodiwa na taarifa za kikao hiki zitatumika kwenye mchakato wa kuchunguza unyanyasaji wa kingono. Taarifa za kikao hiki ziwe siri, lakini wale walioko kwenye kikao hiki wajue, na pia, Mkurugenzi, Askofu, mwanasheria wa TRC, na MEG nao wajulishwe; taarifa hizi zisiwekwe wazi kwa watu walioko nje ya kikao isipokuwa hawa waliotajwa hapo juu.”
 • MEG au mteuliwa atakutana na mshtakiwa na kumweleza kwamba kumekuwa na shtaka la unyanyasaji wa kingono au utovu wa nidhamu. Usitoe maelezo mengi. Mjulishe mtuhumiwa kuwa uchunguzi unaendelea.
 • Uongozi umpatie mtuhumiwa likizo yenye malipo.
 • MEG au mteuliwa (atakutana na) mleta au waleta mashtaka.
 • MEG au mteuliwa atakutana na mleta tuhuma ili kupata taarifa kutoka kwake.
 • Hakiki vielelezo vilivyokusanywa tokana na uchunguzi. Mwanasheria anaweza kuhakiki taarifa zilizokusanywa.
 • MEG au mteuliwa atatoa uamuzi kuonyesha kama tuhuma zilizotolewa zinafikia kwenye kiwango cha unyanyasaji wa kingono au kuleta mazingira ya uhasama wa kikazi.
 • MEG au mteuliwa atakutana na kumjulisha mshitaki kuhusu uamuzi uliotolewa.
 • MEG au mteuliwa atakutana na kumjulisha mshtakiwa kuhusu uamuzi uliotolewa.
 • Mkurugenzi kwa kushirikiana na MEG atatekeleza maamuzi yaliyotolewa kutokana na uchunguzi. Kuna uwezekano wa kuwa na maamuzi ya aina tatu: 1. Kutokuchukua hatua zozote, ila mtuhumiwa achukue tena mafunzo ya unyanyasaji wa kingono. 2. Au, uundwe mpango wa kumrekebisha mtuhumiwa ambao utaainisha hatua za kumrejesha katika hali inayotakiwa. 3. Au, aachishwe kazi mara moja kama italazimika.

MAFUNZO

NI LAZIMA, CMC, LMC NA WAFANYAKAZI WA KANISA WACHUKUE MAFUNZO HAYA

SERA YA TRC YA UNYANYASAJI WA KINGONO

kila jamii inapaswa kuunda sera ya unyanyasaji wa kingono katika eneo lao kwa kufuata mwongozo wa sera iliyowekwa na TRC juu ya jambo hili.

Baraza kuu la The River Conference la kanisa la Free Methodist, (“TRC”) limeamua kuunda na kudumisha huduma na mazingira yasiyoruhusu unyanyasaji wa kingono. Hivyo basi, TRC inakataza unyanyasaji wa kingono wa aina zote kwa wafanyakazi na wawakilishi wake wote sehemu zote. Wazee, CMCs, LMCs na wafanyakazi ni lazima wasijihusishe na tabia hizo zilizokatazwa. Mzee yeyote, CMC, LMC au mfanyakazi atakaye bainika kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kingono visivyokubalika, siyo tu atachukuliwa hatua zinazofaa za kinidhamu, lakini pia anaweza kufukuzwa kazi.

Unyanyasaji wa kingono ni kuvunja maslahi ya mtu na kumtolea heshima yake. Unyanyasaji wa kingono unaweza pia kuharibu huduma yenyewe kwa sababu hushusha motisha ya kufanya kazi, na kuleta hali ya kutoheshimiana miongoni mwa wahusika, na kusababisha baraka za Mungu zipungue. Wafanyakazi na wawakilishi kutoka majimboni lazima waruhusiwe kufanya kazi na kutoa huduma katika mazingira ambayo hayaletelezi hisia za kingono ambazo hazikubaliki.

Unyanyasaji wa kingono kazini unamaanisha mambo yafuatayo: kutumia tendo la ngono kama kigezo au hongo ili kumruhusu mfanyakazi kuendelea na kazi au kupandishwa cheo, kuongezewa mshahara, au kupendelewa katika kugawiwa kazi. Pia, mfanyakazi mmoja anapomlazimisha mfanyakazi mwingine kufanya ngono kinyume cha hiari yake, au kukiwa na kutokukubaliana kuhusiana kimapenzi kati ya wawakilishi majimboni, au kutaka kutumia ngono kama hongo, au kusema matusi ya nguoni kwa mfanyakazi mwingine, au kumlazimisha mfanyakazi kufanya ngono kwa nguvu, au kumwangalia mtu kwa lengo la kuamsha hisia za mapenzi.

Unyanyasaji wa kingono uliopigwa marufuku unahusisha haya, lakini haukomei tu, tabia zifuatazo:

 • Kumtaka mtu isivyotakiwa kimapenzi kwa kuonyesha kutaka kufanya naye ngono, kumtongoza, au kuashiria shauku ya kufanya naye ngono
 • Kutumia vielelezo vya kuashiria nia ya kuwa na ngono, mfano kutumia maneno fulani, kuonyesha tendo lenye kumshawishi mwingine kufanya ngono kwa kutumia bango, picha, katuni, michoro, picha zilizohifadhiwa kwenye skrini ya kompyuta/simu au kuonyesha kwa ishara
 • Kumshambulia mtu kwa nguvu kingono, kugusa bila ruhusa, kumshika mtu mwingine kwa nguvu na kuzuia asijinasue, au kumzuia mtu mwingine asifanye kazi yake;
 • Kutumia vitisho na kumlazimisha mtu akubali ombi la ngono kama sharti la yeye kukubaliwa kuendelea na ajira, au kama kigezo cha kusaidia kuepuka asipate hasara fulani, au kutumia ombi la ngono kama sharti la kupewa mafao kazini.
 • Kulipiza kisasi kwa anayetoa taarifa au mtu anayetishia kutoa taarifa za unyanyasaji wa kingono.

 

Mzee yeyote, CMC, LMC au mwajiriwa yeyote ambaye anafahamu juu ya tukio lolote la unyanyasaji wa kingono anapaswa kutoa taarifa mara moja juu ya tuhuma hizo kwa msimamizi wake (Mkurugenzi, Msaidizi wa Mkurugenzi). Mwajiriwa au mwakilishi wa jimbo yeyote anayeamini kuwa ameadhirika kutokana na unyanyasaji wa kingono anapaswa kufanya vivyo hivyo. Ikiwa Mwajiriwa au mwakilishi wa jimbo hana ujasiri kulizungumzia swala hilo kwa msimamizi au ikiwa msimamizi wake hayupo, mwajiriwa au mwakilishi wa jimbo anapaswa kutoa taarifa za tuhuma hizo mara moja kwa Mkurugenzi wa  The River Conference la Kanisa la Free Methodist. Waajiriwa au wawakilishi wa jimbo wanahimizwa kutoa taarifa mara moja juu ya tabia za aina hii.

Taarifa au malalamiko yoyote yanapaswa kuwa na maelezo ya undani juu ya tukio au matukio ya unyanyasaji wa ngono, kwa mfano, majina ya watu waliohusika na majina ya mashahidi wowote. Uchunguzi wa kina na usio na upendeleo juu ya tuhuma hiyo utafanyika mara moja na utashughulikiwa kwa usiri mkubwa kadri iwezekanavyo. Wahusika wataarifiwa juu ya matokeo ya uchunguzi, mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Iwapo itabainika kuwa unyanyasaji ulio kinyume na sheria umetokea, hatua madhubuti za kinidhamu zenye lengo la kuleta uponyaji zitachukuliwa mara moja zikizingatia mazingira ya mahali tukio lilipotokea.

TRC haitalipiza kisasi dhidi ya Mzee, CMC, LMC au mwajiriwa yeyote kwa sababu ya kutoa taarifa za malalamiko, na haitavumilia au kuruhusu uongozi, waajiriwa, wafanyakazi wenzake na mwathirika au wawakilishi wa majimbo kulipiza kisasi.

Kila mzee, CMCs, LMCs na waajiriwa wote, watatakiwa kutia saini hati ya kuonyesha kukubali kwamba, wamesoma, wameelewa na watatii sera iliyotajwa.

Kila mzee, CMCs, LMCs na kila mwajiriwa, anatakiwa kuchukua mafunzo juu ya unyanyasaji wa kingono yatolewayo na Brotherhood Mutual na watawasilisha uthibitisho wa kumaliza mafunzo yao juu ya unyanyasaji wa kingono yanayotolewayo na Brotherhood Mutual.

Ninathibitisha kuwa nimeisoma sera iliyotajwa hapo juu na kuielewa na nimekubali kufuata maelekezo yake kwa sahihi yangu hapa chini.

 

Jina _____________________________

Sahihi _____________________________

Tarehe _____________________________

V20220815

 

Baada ya kusoma sera hii na kumaliza mafunzo ya kwenye mtandao, tafadhali thibitisha kwamba umesoma na kuelewa sera hii kwa kujaza hapa chini:

 

Sahihi na wasilisho la cheti cha kuchukua mafunzo na kusoma sera ya unyanyasaji wa kingono

Tumia fomu hii kuweka sahihi kwenye fomu na kuwasilisha cheti chako cha mafunzo ya mtandaoni ya Brotherhood Mutual

MM slash DD slash YYYY
Mwezi/siku/mwaka
Anuani pepe (lazima)(Required)
Jina lako (lazima)(Required)
Max. file size: 100 MB.
Chagua faili. Ukubwa wa faili unaoruhusiwa: 100 MB